TTCL

Habari

WATANZANIA KATIENI BIMA MALI ZENU – DK. SAQWARE.

on

Kamishna wa Bima nchini Dk. Baghayo Saqware akitoa salam za rambirambi katika  msiba wa Baba mzazi wa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Bima Nyanda za juu kusini, Elia Kajiba Marehemu Paul Kajiba wakati wa Ibada iliyofanyika katika Kanisa la Moravian Mbeya mjini.Kamishna wa Bima nchini Dk. Baghayo Saqware (kushoto) akifuatilia Ibada ya mazishhi ya  Baba mzazi wa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Bima Nyanda za juu kusini, Elia Kajiba Marehemu Paul Kajiba iliyofanyika katika Kanisa la Moravian Mbeya mjini na kuzikwa makaburi ya Nonde. Baadhi ya Waombolezaji wakiwa kanisani wakifuatilia Ibada ikiendelea.

WATANZANIA wametakiwa kuwa na utaratibu wa Kukatia Bima Mali zao ili kujikinga na hasara pindi majanga mbalimbali yanapotokea na kupelekea vilio kwa Wahanga.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Kamishna wa Bima nchini Dk. Baghayo Saqware alipokuwa akizungumza na mtandao huu kuhusu mwitikio wa Watanzania katika kukata Bima za Mali zao alipokuwa akihani msiba wa Baba mzazi wa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Bima Nyanda za juu kusini, Elia Kajiba Marehemu Paul Kajiba.
Kamishna huyo alisema kuwa na Bima kunamuondolea hofu ya kupoteza Mali kutokana na kuwa na uhakika wa kuweza kulipwa fidia na Kampuni ya Bima baada ya aidha kupata ajali ya Moto,tetemeko la ardhi au kimbunga kinachoweza kusambaratisha Mali pamoja na mafuriko.
Alitolea mfano Wahanga wa Soko la Sido jijini Mbeya ambao walikumbwa na janga la Moto lililopelekea kuteketeza Mali na bidhaa mbalimbali zilizokuwemo kwenye maduka yao lakini waliokuwa na Bima waliweza kulipwa na hatimaye kupata mitaji ya biashara zao.
Aliongeza kuwa kuna aina nyingi za Bimaambazo kila Mtu anaweza kukata ikiwemo Bima ya Mali, ajali, Maisha na Bima ya Afya kwa ajili ya kuwezesha familia kupata matibabu muda wowote wanapougua.
Hata hivyo akitoa salam za rambi rambi katika ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Moravian Usharika wa Mjini jijini Mbeya na kuzikwa katika makaburi ya Nonde, Kamishna huyo aliwataka jamii kuishi kwa upendo na kufuata matendo mema ya Marehem.
Naye Meneja wa Bima Kanda ya Nyanda za juu kusini, Consolata Gabone alisema upendona mshkamano mahala pa kazi ni ishara ya ushirikiano ambao umeoneshwa na kuguswa na Kamishna hadi kuhudhuria ibada ya mazishi.
“Sio Kawaida kwa Kamishna kuja huku mkoani kushiriki msiba wa kufiwa kwa mfanyakazi wake kwani alikuwa na uwezo wa kutuma mwakilishi hivyo tunajifunza kuishi kwa upendo na mshikamano sehemu zetu za kazi” alisema Gabone.

UJUMBE KWA FACEBOOK