TTCL

Habari

WAZIRI MKUU AWATABIRIA KIAMA WATAKAOWAPA MIMBA WANAFUNZI

on

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nasuli mjini Namtumbo wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. amewatahadharisha watu wanaotamani kuwachumbia na kuwaoa wanafunzi kwamba watakiona cha moto.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi wa Sekondari Nasuli

Waziri Mkuu akizungumza na wananchi wa Namtumbo

Baadhi ya wananchi wa Namtumbo wakimsikiliza Waziri mkuu Kassim Majaliwa wakati alihutubia mkutano wa hadhara jana jioni.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa akisikiliza taarifa ya ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao iliyosomwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Namtumbo Christopher Kilungu

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Namtumbo(katikati) akijadiliana jambo na Ofisa Mipango wa Halmashauri hiyo Gwakisa Mwasyeba(kulia) wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

 

Waziri Mkuu Majaliwa amesema yoyote anayewatamani wanafunzi kwa kuwachumbia hata kuwaoa serikali haitachelewa kuwachukulia hatua kwa kuwafunga miaka 30 jela.

Akizungumza mara alipokutana na wanafunzi wa shule ya sekondari.ya Nasuli iliyopo Namtumbo mkoani Ruvuma aliwataka wanafunzi hao kutoshawishika na propaganda za wanaume.

“Kataeni Lifti za madereva wa Bodaboda, waiteni lile jina la FATAKI,.msikubali kukatishwa ndoto zenu,serikali ilo pamoja nanyi”Alisema Waziri Mkuu.Majaliwa.

Awali Waziri Mkuu alifungua ghala la kuhifadhia mazao lenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani 200 lililoghatimu Tsh Mil 413.

Na Rashid Mkwinda

UJUMBE KWA FACEBOOK