TTCL

Habari

WENYE KISUKARI MBEYA WAUNDA CHAMA

on

Muuguzi mkuu Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Thomas Isdory akitoa hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospitali hiyo wakati wa uzinduzi wa Chama cha WenyeKisukari Tawi la Rufaa

Dk. Jamil Kajuna ambaye ni mtaalam wa magonjwa ya Kisukari kwa Watoto akielezea dalili za ugonjwa wa kisukari wakati wa uzinduzi wa Chama cha Wenye Kisukari Tawi Tawi la Rufaa Mbeya.

Mshereshaji Guydon Makulila  mtoa dawa za usingizi akiongoza hafla ya uzinduzi wa Chama cha wenye kisukari Tawi la Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya akiendesha ratibaMkuu wa Idara ya tiba ya Kisukari katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Dk.Sangare Antony akielezea umuhimu wa Wagonjwa wa kisukari kuwa na Chama ili kubadilishana mawazo.

Mtaalam wa Chakula na Lishe katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Joyce Komba akielezea tiba ya sukari kwa wagonjwa ni kuzingatia ulaji wa vyakula kwa mpangilio.

Baadhi ya wagonjwa wa kisukari wakipata ushauri na vipimo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.

Mhudumu wa Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya akimchukua damu mwananchi kwa ajili ya vipimo vya Sukari

Baadhi ya Wagonjwa wa Kisukari ambao ni Wanachama wa Chama cha Wenyekisukari Tawi la Rufaa wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Chama hicho.
WAGONJWA wa Kisukari nchini wametakiwa kuzingatia ushauri wa Wataalamu kuhusu ulaji wa vyakula vya lishe na ufanyaji wa mazoezi hali itakayopelekea kupona kabisa kwa ugonjwa huo.

Rai hiyo ilitolewa juzi na Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Thomas Isdory alipomwakilisha Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk. Godlove Mbwanji wakati wa ufunguzi wa Chama cha Wenye kisukari Tawi la Hospitali.

Alisema Wagonjwa wa kisukari wanapaswa kuzingatia ushauri wa Wataalamu kwani wao wanatakiwa kupewa elimu zaidi namna ya ulaji wa vyakula ili kuweza kumuda na kufahamu jinsi ya kuifanya sukari iliyopo mwilini kuwa katika kiwango stahili bila kuleta madhara.

Alisema kupitia Chama cha Wenye kisukari itachangia wanachama wenyewe kwa wenyewe kutembeleana na kupeana elimu kuhusu ugonjwa wa kisukari na namna ya kukabiliana nao.

Aliongeza kuwa Hospitali ya Rufaa inajitahidi kuendelea kuboresha huduma kila siku ili wateja wao ambao ni wagonjwa waweze kupata matibabu yanayotakiwa na kwakati husika ikiwemo upatikanaji wa Dawa na vifaa tiba.

Awali Mkuu wa Idara ya Tiba ya Kisukari katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Dk. Sangare Antony alisema Wizara ya Afya iliagiza kila wenye magonjwa ya kudumu kuunda vyama vyao wakiwemo wenye kisukari jambo lililofanyika sasa.

Alisema lengo la kuunda chama cha wenyekisukari ni kuweza kujadili namna ya kukabiliana na changamoto mbali mbali wanazokumbana nazo katika kupata matibabu pamoja na kutambuana wenyewe kwa wenyewe.

 

UJUMBE KWA FACEBOOK