TTCL

Habari

WRP WATOA MSAADA WA VIFAA KWA JESHI LA POLISI MBEYA

on

Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Mbeya, Costantine Mushi akikata utepe kuzindua msaada wa vifaa vya kutunzia kumbukumbu kwa Jeshi la Polisi kitengo cha dawati la Jinsia vilivyotolewa na Shirika la WRP. Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Mbeya, Costantine Mushi akitoa hotuba katika hafla ya kupokea  msaada wa vifaa vya kutunzia kumbukumbu kwa Jeshi la Polisi kitengo cha dawati la Jinsia vilivyotolewa na Shirika la WRP. Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la WRP, Joseph Ng’weshem akielezea aina ya msaada walioutoa kwa jeshi la Polisi Mkoawa Mbeya katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga akishukuru kwa ajili ya msaada wa vifaa kutoka WRP Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Mbeya, Janeth Masangano akielezea changamoto ambazo dawati hilo linakabiliana nalo ikiwemo ukosefu wa vifaa kabla ya kupokea msaada kutoka WRP Mratibu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Mbeya, Debora Lukololo akielezea umuhimu wa wadau katika kukomesha na kukabiliana na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia. Kaimu Mkurugenzi wa huduma za jamii kutoka WRP, Angelina Mchome akizungumza namna WRP inavyoshirikiana na Jeshi la Polisi katika kukabiliana na matukio ya Ukatili wa kijinsia kwenye jamii Kaimu Mkurugenzi wa huduma za jamii kutoka WRP, Angelina Mchome akipokea tuzo kutoka kwa mgeni rasmi, Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Mbeya iliyotolewa na Jeshi la Polisi kutokana na kutambua mchango wao. Kaimu Mkurugenzi wa huduma za jamii kutoka WRP, Angelina Mchome akionesha cheti maalum walichopewa na Jeshi la Polisi baada ya kutambua mchango wao katika kupambana na ukatili wa kijinsia Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la WRP, Joseph Ng’weshem akimkabidhi Laptop Kaimu KatibuTawala Mkoa wa Mbeya kwa niaba ya Jeshi la Polisi.KaimuKatibu tawala Mkoa wa Mbeya Costantine Mushi akimkabidhi Laptop Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya akionesha Laptop aliyokabidhiwa kutokana na msaada kutoka WRP Baadhi ya Maafisa wa Polisi  na wadau wakishuhudia makabidhiano ya vifaa vya kutunzia kumbukumbu kwa Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsia. Baadhi ya Maafisa wa Polisi  na wadau wakishuhudia makabidhiano ya vifaa vya kutunzia kumbukumbu kwa Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsia. Baadhi ya Vifaa vilivyotolewa na WRP kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kitengo cha Dawati la Jinsia. Baadhi ya Maafisa wa Polisi  na wadau wakishuhudia makabidhiano ya vifaa vya kutunzia kumbukumbu kwa Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsia.

SHIRIKA la Walter Reed Program (WRP) Tanzania limetoa msaada wa vifaa vya utoaji na utunzaji wa kumbukumbu  kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.

 

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kaimu Mkurugenzi wa WRP, Joseph Ng’weshem alisema msaada huo unagharimu fedha za kitanzania shilingi  Mil 10,224,000.

 

Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni Skana 3,Kamera 3,Kompyuta za mezani (Desktop) 3,Kompyuta mpakato (laptop) 1, Printa 1 na Flashi 3.

 

Alisema vifaa hivyo ni kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Dawati la Jinsia la Jeshi la Polis katika kupambana namatukio ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.

 

Awali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga mbali na kushukuru kwa msaada huo alisema Shirika limeonesha mfano wa ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi na wadau katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.

 

Alisema vifaa hivyo vitasaidia kuboresha ufanisi wa kazi za Jeshi la polisi katika kushughulikia na kutatua masuala ya ukatili wa kijinsia pindi yanapotokea kwani nyaraka na kumbukumbuzitakuwa zikihifadhiwa vizuri.

 

Naye mgeni rasmi katika hafla hiyo, Katibu tawala msaidizi Mkoa wa Mbeya anayeshughulikia Serikali za Mitaa, Costantine Mushi kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya alitoa wito kwa Jeshi la Polis kutumia msaada huo kama ilivyokusudiwa.

 

Alisema vifaa hivyo ni kwa ajili ya kuimarisha madawati ya kijinsia kwa kutunzia kumbukumbu na vielelezo vya matukio ya ukatili ili visaidie katika kutoa ushahidi mahakamani.

 

Alisema ni marufuku kubadili matumizi ya vifaa hivyo tofauti na malengo yake hivyo ni jukumu kwa wahusika kuhakikisha wanatunza vizurina kuvitumia kwa usahihi.

UJUMBE KWA FACEBOOK